Michezo

 

Mchezaji wa Lipuli, Adam Salamba amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba kwa msimu ujao

 ALIYEKUWA mshambuliaji wa Lipuli FC ya Iringa, Adam Salamba amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Klabu ya Simba kwa dau la Shilingi milioni 30.Simba wameinyaka saini ya Salamba baada ya kuwazidi kete Yanga na Azam waliokuwa wakimuwania mchezaji huyo.Salamba amesaini mkataba huo mbele ya Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ na baadaye kukutana na Mohamed Dewji, Bilionea anayetarajia kuwekeza ndani ya Simba kitita cha Sh bilioni 20.

WAZIRI MWAKYEMBE AFANYA UTEUZI 

WA MWENYEKITI WA BODI YA FILAMU NCHINI 



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amemteua Prof. Frowin Paul Nyoni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania pamoja na wajumbe wapya sita wa bodi hiyo.
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Wizara hiyo na kusema uteuzi huo umeanza kufanya kazi rasmi Aprili 18, 2018 na wataitumikia bodi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kwa taarifa kamili soma hapa chini..

Comments

Popular posts from this blog