KANISA LAPIGA MARUFUKU UVAAJI WA SHELA ZA HARUSI Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, limewapiga marufuku wanawake wajawazito kuvaa shela wakati wa kufunga ndoa kwa madai vazi hilo ni alama ya ubikira kwa mwanamke na sio vinginevyo. Hayo yamesemwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresa, Padre Festus Mangwangi wakati akiweka mkazo juu ya tamko lililotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Isaack Amani, wakati akiadhimisha misa ya shukrani iliyofanyika Jumapili iliyopita, baada ya kuteuliwa kwake na Baba Mtakatifu Francis kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo. Kabla ya uteuzi huo uliotangazwa Desemba 27 mwaka 2017, Askofu Mkuu Amani alikuwa Askofu wa Jimbo la Moshi na kusema haitakiwi kwa mwanamke yeyote ambaye anajijua ni mjamzito kuvaa shela kipindi anafunga ndoa kwa kuwa vazi hilo linavaliwa na mwanamke asiyemjua mwanaume (bikra). Aidha, Padre Festus Mangwangi amewataka wazazi kuwafundisha watoto wao wa kike kutunza miili ya
Comments
Post a Comment